Muigizaji wa filamu kwa hapa nchini Tanzania Kulwa Kikumba (Dude) anasema kuwa pamoja na baadhi ya wasanii kumjengea bifu kwa kutoandamana nao katika mambo yao ambayo kwake yeye anaona kuwa hayana faidi katika jamii wala kwa wasanii wenyewe zaidi kwa baadhi wanaoendesha kampeni hizo hatosita kusema ukweli unaolenga kujenga tasnia hii na si vinginevyo.
Dude anasema kuwa kwa hivi sasa tayari kuna makundi yasiyo rasmi katika tasnia ya filamu huku baadhi ya watu waliofanya vibaya katika maisha wakikimbilia katika tasnia hii na kufanya ni kichaka cha wale wote ambao wameshindwa kufanya shughuli zao, na wanapofika huku wanakuja kwa lengo moja tu kuuza sura ili kupata Mapedje na Mashuga mami hawana sanaa zaidi ya kazi hiyo ya kuuza sura anasema Dude.
“Filamu hazilipi kwa msanii ndiyo maana maisha yetu kwa asilimia kubwa wasanii wengi tunaishi kwa Mizinga, wenzetu wanaopenda kutembea sehemu za starehe ndiyo maisha yao, akisalimiwa tu lazima utasikia ebwana nipo hapa nakunywa Nduvu, kandovu kamoja bwana huku akinyosha kidole kimoja kama ishara ya msisitizo wa kununuliwa bia lakini msanii huyu huyu akiulizwa filamu vipi utasikia filamu zinalipa bwana” Anasema kwa uchungu Dude.