Google PlusRSS FeedEmail

FILAMU YA SHOGA YAACHIWA HURU KUINGIA SOKONI

Filamu iliyokuwa awali ikiitwa Shoga imeruhusiwa kuingia sokoni baada ya kubadilisha jina kutoka Shoga na kuwa Shoga Yangu, filamu ilisimamishwa na Bodi ya Ukaguzi wa filamu kutoka na matatizo yaliyokiuka maadili na utamaduni wa Tanzania, hatua iliyofanya filamu hii kuzuiwa kutoka na kuingia mtaani jambo liloibua maneno maneno kutoka kwa baadhi ya wasanii wakiona kama kuna uonevu.
Lakini baada ya wahusika kufika bodi na kuelezwa taratibu na sheria ya iliyounda Bodi hii ya mwaka 1976 namba 4 inaeleza kuwa kuna hatua za kufuata kabla ya kuingia Location kupata kibali cha kurekodi, ukaguzi wa muswada ambao wahusika ni Bodi na kabla ya filamu kuingia sokoni kukaguliwa na kupewa daraja, hazi ni baadhi ya taratibu za kufuatwa, nimeamua kuziandika ili watayarishaji wa filamu watambue.
Katibu wa Bodi  alisema kuwa filamu iliyoruhusiwa ni Shoga Yangu na ndiyo wanayoijua, filamu hii imebadilishwa jina hilo kutokana na muonekano wa jina la kwanza lakini kitu kingine kulikuwa na picha ambazo si sahihi kuonekana katika maadili ya kitanzania zaidi katibu wa Bodi anasema.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging