Mwisho Mwampamba,naye alitiwa mbaroni katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Dar es Salaam baada ya kumwagia mvua ya matusi muigizaji wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel
Tukio hilo lilitokea huko Kijitonyama,Dar na chanzo cha kisa hicho ni kutoelewana baada ya Mwisho kudaiwa kukiuka masharti ya mkataba baina yake na Aunt Ezekiel aliyemtoa jijini Arusha kwa ajili ya kushiriki kucheza filamu yake ya Men’s Day Out na Juhudi za Aunt Ezekiel kubembeleza Mwisho ziliishia kuambulia matusi ya nguoni na kuamua kuripoti Oysterbay na baadaye akakabidhiwa askari waliokwenda kumkamata Mwisho na alitoka usiku kwa dhamana huku akitakiwa kuripoti siku iliyofuata kwa ajili ya maelezo zaidi