LINEX NA SUMA LEE KUTOKA NA BODABODA
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya ‘Bongo fleva ‘ Linex na Suma Lee wanatarajia kutoka na ngoma mpya hivi karibuni iitwayo Bodaboda
Wakizungumza na mwandishi wa habari hii kwa nyakati tofautitofauti Linex alisema kuwa ameamua kufanya ngoma moja na Suma Lee kwani ni mwanamuziki anayejua nini anafanya na yuko teyari kufanya kazi muda wowote ule
Alisema kuwa ujio huo wa kufanya ngoma moja na Suma Lee wameipa jina la Kigo Tanga ikiwa na maana kuwa Suma Lee anawakarisha Tanga na yeye anawakilisha Kigoma
Linex alisema kuwa teyari wamesharekodi ngoma hiyo katika studio ya fundi Samweli iliyopo Kibaha na kuwataka wapenzi wao wakae mkao wa kuipokea ngoma hiyo
Kwa upande wake Suma Lee alisema kuwa kwake ni faraja kubwa kwa kuona kuwa aliweza kuifanyia kazi wazo la ngoma hiyo ambapo wazo hilo lilikuja kwa siku moja
“Tulikuwa safarini mimi na Linex ndipo mzuka ukaja tukashuka mistari na tukaona inafaa ndipo tulipoamua kushuka studio kibaha tukarekodi nyimbo hiyo kwa siku moja” alisema Suma Lee
Aliongezea kuwa anaamini ngoma hiyo itafanya vizuri kwani inahisia na uwalisia , pamoja na hayo alijitamba kuwa hawajawahi kutoa ngoma ambayo haijawahi kufanya vizuri