NI KWELI BI KIDUDE KUACHANA NA MUZIKI
Mwimbaji mkongwe wa muziki wa taarabu hapa nchini Hadija Binti Baraka maarufu kama Bi Kidude amedaiwa kushawishiwa na wadau wake achana na mambo ya kupanda jukwaani kuimba ,hiyo inatokana na ukongwe wake hali inayomfanya ashindwe kujimudu ikiwemo kupanda jukwaani kuimba kama wanavyofanya wengine wenye kujiweza
Habari kutoka kwa mtu wa karibu na Bi Kidude zinazema upo mpango wa kuandaa tamasha maaalumu kwa ajili ya kumuaga muimbaji huyo ili achane na muziki wa taarabu nchini
Alisema fedha zitakazopatikana katika shoo hiyo zitaingia katika mfuko wa bibi huyo kuliko kumuacha kama anavyofanya sasa na kuganga njaa katika majukwaa mbalimbali ya muziki