SAM WA UKWELI KUACHIA NGOMA MPYA
Nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini , Salim Mohamed ‘Sam wa Ukweli’ yupo katika hatua za mwisho kuachia kibao chake kipya kinachokwenda kwa jinala ‘Najua’
Akizungumza jijini Dar es Salaam Sam alisema anakamilisha uandaaji wa wimbo huo ambao anaamini utafanya vizuri kutokana na ujumbe uliomo
Alisema anatarajia kuachia ‘audio’ na video vyote kwa pamoja ili kuwaletea ladha mashabiki wake, ambao wanaamini wanaisubiri kwa hamu kazi hiyo
“Naomba mashabiki wangu waendelee kunipa sapoti katika kazi zangu kwani kuna vitu vingi ambavyo nimewaandalia na wimbo huu utaanza kuonekana na kusikika mwishoni mwa wiki ijayo” alisema