AY KUHAMASISHA MRADI KUSAIDIA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM
Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel, kupitia kitengo chake cha huduma kwa jamii na Msanii wa Bongofleva, Ambwene Yesaya 'AY' wameanza mchakato wa kutembelea shule zitakazo nufaika na mradi maalum wa kusaidia watoto wenye mahitaji maalum ili kujionea changamoto zinazowakabili na kuwahimiza watanzania kuchangia mradi unaoendeshwa kwa ushirikiano wa Baraza la Maendeleo ya Vitabu Tanzania (BAMVITA)
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari Dar es Salaam na Ofisa Mawasiliano na Matukio wa kampuni hiyo, Dangio Kaniki ilielezwa kwamba kampuni hiyo ikiwa na balozi wake, AY itatembelea shule zilizopo Dar es Salaam pamoja na mikoani na kubainisha matatizo wanaoyokumbana nayo ili kuona namna ya kuwasaidia
Alisema shule za wanafunzi zenye mahitaji maalum zinahitaji vitendea kazi ili kuwafanya wanafunzi hao kuweza kupatiwa elimu inayostahili
Akizungumza mara baada ya kutembelea shule za msingi Sinza Maalum,balozi AY alisema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kuongeza kiwango cha elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum