Google PlusRSS FeedEmail

SKENDO NYINGINE BONGO MOVIES

Bosi wa Nidhamu wa Klabu ya Michezo ya Waigizaji wa Bongo ‘Bongo Movie’, Heriety Chumira amejivua gamba kwa kuachia nafasi yake hiyo.Hii ni skendo nyingine ndani ya klabu hiyo kwa sababu, Heriety alisema ameamua kuachia kiti hicho kwa sababu amechoshwa na tabia za wasanii hasa akina dada walioko kwenye klabu hiyo ambao matendo yao yamekuwa yakimdhalilisha hata yeye ambaye ni mke wa mtu.“Kama mama wa nidhamu wa Bongo Movie, nimekuwa nikipokea malalamiko ya vitendo vya hawa wasanii, hasa wa kike na huwa vinaniumiza sana.

“Hivyo nimeamua kuachia ngazi ingawa sijatoa tamko rasmi kwa uongozi kwa sababu mpaka muda huu klabu yenyewe haijakaa sawa, kila mtu ana mambo yake,” alisema.

Akaongeza: “Unajua wasanii wana mambo mengi ya ajabu, ukiwauliza wanakwambia wanasingiziwa, wakati mwingine ukiwakemea wanakuchukia, naona nimeshindwa.” Siwezi kuwataja watanijia juu, lakini wanajijua wenyewe kwani hawaishi matukio kila kukicha. Kwa kweli inabidi wabadilike vinginevyo watajutia
Heriety alisema siku moja wakiwa mazoezini, baadhi ya wasanii walikwenda uwanjani na nguo zilizokuwa zikionesha maumbile, alipowasema siku iliyofuata walivaa magauni ya kumkomoa.

“Siku moja walikuja mazoezini na nguo za ajabu, unaona maumbo, nikawasema, kesho yake wakaja na magauni marefu, nilipowauliza kwa nini wamekuja na magauni mazoezini, wakajibu kwa kejeli ‘si ndo unavyotaka tuvae’, kweli sikufurahi na nimevumilia mengi sana,” alisema Heriet “Mimi sijajitoa Bongo Movie ila nimeamua kuachia nafasi ya kusimamia nidhamu, apewe mtu mwingine naye aonje joto la jiwe.” alimaliza Heriety.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging