CHRIS BROWN KUTOA VIDEO YA MAPENZI NA RIHANNA
Mwimbaji wa R&B Chris Brown anatarajia kuachia video yake mpya itakayoondoa utata ulioko juu ya mapenzi yake na muimbaji Rihanna yaliyosababisha kutengana na mpenzi wake Karrueche
Inaelezwa kuwa wawili hao walipiga picha za video hiyo ambayo imewaonesha wako chakali kwa pombe huku Brown akivuta na baadae kuwekwa kwenye mitandao yao binafsi
Video hiyo imepigwa wakati wawili hao walipokuwa kwenye klabu moja ya usiku ambako inamuonyesha Brown akisema "nimekunywa kidogo lakini sina ugomvi na mtu na ni muaminifu"
Video hiyo imeelezwa kwamba jana iliwekwa kwenye mtandao wa Twitter na Brown ikipambwa na maneno yanayotoa picha kuwa wawili hao ni wapenzi