Google PlusRSS FeedEmail

DULLY SYKES PROFILE, ANATAMBA NA TUNGO, AMILIKI STUDIO MBILI,ANATAMBA NA KIBAO CHA 'MTOTO WA KARIAKOO'



Ukizungumzia majina matano ya wanamuziki waanzilishi wa muziki wa bongo fleva nchini Tanzania hauwezi kuliacha kulitaja jina la mwanamuziki Dully Sykes ambaye ameanza muziki wake miaka 16 iliyopita

Dully ambaye ni mahiri katika mashahiri ya muziki wa kizazi kipya huku akiwa na uwezo wa kuwatega mashabiki wake kwa kila tungo anayeitunga kwenye muziki wake utakamata katika vichwa vya mashabiki wake

Dully mwenye malengo ya kupeleka muziki wa Tanzania katika anga za kimataifa huku kutoa albamu kitambo ni msanii anayejua nini anachokifanya na nini anachokitaka katika anga za muziki hususani muziki wa kizazi kipya

Anajulikana kwa kuwa na tungo nyepesi lakini ambazo hukamata ndani ya muda mfupi na kwa aina yake, historia inatukumbusha enzi za Nyambizi na Julieta ni nyimbo ambazo zilikamata na kuteka mashabiki wa muziki kwa kile kinachozungumziwa ndani ya nyimbo hizo

Dully aliyetoka na albamu tatu mnamo mwaka 2003, kwa hivi sasa ameacha kutoa albamu kwa kile kinachodaiwa kuwa albamu hazilipi katika soko la muziki wa kizazi kipya

Dully ambaye alipata nafasi ya kuzungumzia muziki wake kiujumla alisema kuwa muziki kwake ni maisha anayoyaishi kila siku

Anasema kuwa muziki ni kazi yake hivyo huhakikisha kile anachokifanya ni cha kuwajali mashabiki wake hivyo huhakikisha kufanya vizuri katika shoo zote anazoalikwa ili kukonga nyoyo za mashabiki wake

Dully anasema kwamba kwa sasa anamiliki studi mbili pamoja na  bendi moja hii yote ni kwa ajili ya kuboresha muziki wake na mashabiki kupata radha nzuri kwa kile wanachokikusudia kutoka kwake

Akizungumzia kuhusu studio ya Dhahabu Records ambayo inamilikiwa na yeye mwenyewe iliyopo Tabata jijini Dar es salaam imeshatoa nyimbo kibao zikiwemo za kwake na za wasanii wengine

Dully ambaye ameonekana kuwa na mchango mkubwa sana kwa wasanii chipukizi ambao wanahitaji msaada kutoka kwake wa namna moja au nyingine amekuwa msaada kwa wasanii hao

Dully Katika Vipindi mbalimbali nimeweza kusikia wasanii wapya wakimtaja Dully Sykes kuwa alitoa support ya aina fulani katika mafanikio mpaka hapo walipofikia na wengine wanasema amewaonyesha njia ya kufanya makubwa zaidi katika tasnia ya muziki

kudhihirisha hilo hata Diamond katika show ya Salama Mkasi TV ajasita kumpa sifa Dully kuwa na yeye alikuwa na mchango mkubwa katika kazi yake ya sanaa mpaka hapo alipofikia

Hii ni Sifa nzuri kwa mwanamuziki Huyu Mkongwe na ni mfano unaobidi uigwe na wasanii wengine wakongwe kwani kila mtu anahitaji msaada kwa mwengine ili akamilishe mafanikio yake

Dully ambaye anatamba na vibao vingi ikiwemo shikide, na sasa anatamba na 'mtoto wa kaliakoo'ni nyimbo ambayo sasa imeshika kasi na inafanya vizuri hadi kwenye top ten katika vipindi mbalimbali vya redio

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging