Mwimbaji machachari Rihanna Fenty na Nicki Minaj wanaongoza
kuwania tuzo nyingi za muziki Marekani (AMA) waimbaji hao mmoja anawania tuzo
nne tofauti katika kipengele cha muimbaji bora wa kike wa pop/rock
Rihanna pia anagombea tuzo ya msanii bora wa mwaka, muimbaji
bora wa kike wa miondoko ya soul/ R&B pia albamu yake ya Talk That Talk
inawania tuzo ya albamu bora ya mwaka ya miondoko ya soul/R&B
Nyota huyo anamatumaini ya kufanya vizuri kuliko ilivyokuwa
hivi karibuni kwenye tuzo za video bora za MTV (VMA)ambavyo alishinda moja tu
katika vipengele vitano alivyotajwa
Nicki ni mkali mwingine anayenyemelea ushindi wa kishindo
katika tuzo za AMA kwa upande wa msanii bora wa rap/hip pop na albamu bora ya
pop/rock,ameingia katika vipengele vyote vya tuzo hiyo kupitia albamu yake Pink
Friday Roman Reloaded