MSANII wa muziki wa kizazi kipya mwenye nyimbo za maneno ya shombo kwa baadhi ya wasanii hususani wa filamu nchini Ney wa Mitego mungu amemjalia kwa kupata mtoto wa kiume aliyempa jina la Khairain
Akizungumza na jarida hili la Maisha alisema kuwa hayuko teyari kumuweka wazi mwanamke aliyezaa naye kwa kigezo kuwa muda bado haujafika na ukifika kila kitu kitakuwa wazi
Alisema mwanamke aliyezaa naye ni wa kawaida na hafahamiki katika tasnia ya sanaa kiujumla, kwa hali hiyo inamsababisha yeye kuishi vizuri na mwanamke huyo bila ya matatizo yoyote hususani skendo zinazosababisha kuvunjika kwa mahusiano mengi ya wasanii walio wengi
"Nimefurahi kupata mtoto wa kiume kwani ni moja ya ndoto zangu, namshukuru mwanamke aliyenizalia mtoto huyo, muda ukifika nitamuweka wazi na kufunga naye ndoa kwani ndoa ni mipango ya baadaye kidogo mpaka tujipange " alisema Ney wa Mitego
Wakati huo huo Ney alizungumzia picha zake zinazoonekana kuzagaa katika mitandao ya kijamii akionekana yeye na msanii wa Bongo Muvi 'Nisha' wakiwa faragha
Alisema kuwa chanzo cha picha hizo ni za filamu yao mpya ambayo inatarajia kutoka hivyi karibuni sokoni, katika filamu hiyo alicheza yeye na Nisha wakiwa faragha na hawakupanga kuongelea chochote juu ya picha hizo
"Picha hizo zimesambaa mitandaoni kwa bahati mbaya kwa sababu zilikuwa kwenye simu ya Nisha bahati mbaya alipata ajari na simu yake kupotea hivyo baadhi ya watu wakaziona hizo picha na wakaamua kuzisambaza kwenye mitandao bila ya kujua madhumuni ya picha hizo" alisema Ney wa Mitego