SHETTA ATAMBULISHA BONGE LA BWANA
MSANII wa muziki wa kizazi kipya ambaye ni rais wa Darstamina Shetta mwisho wa wiki hii alitambulisha single yake mpya ya Bonge la Bwana na style yake mpya ya kiduku ya 'swaga na tetemesha' pamoja na Website iliyotambulika kwa jina la www.shettamusic.com jijini Dar es Salaam
Uzinduzi huo ulipambwa na wakali kibao kama Roma, Shilole, Suma Mnazaleti, Ney wa Mitego, Makomando, Pasha, Young Dee, Nyandu Tozi na kundi jipya la Dada Rashac,
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Shetta alisema kuwa nia ya uzinduzi na kumili website yake ni njia ya kujikuza kimataifa na kujitangaza katika soko la kimataifa la muziki
Alisema kuwa ili ujitangaze na kazi zako zitambulike ni muhimu kuwa na mitandao ili utumie zaidi katika kujitangaza na kutangaza kazi zako kimataifa
Wakati huo huo msanii Shilole alifanya shoo ya nguvu katika uzinduzi huo huku kuonekana kukonga nyoyo za mashabiki wake kwa umahiri wake wa kukata kiuno huku akiibua hisia tofauti kwa mashabiki waliohudhuria uzinduzi huo
Akizungumza baada ya uzinduzi huo alisema kuwa kushambulia jukwaa ni kazi yake kwani anafanya kazi hiyo kwa ajili ya kuwaburudisha wasanii
"Mimi ni kazi tu hapa sina lingine na watu wananijua mashabiki wangu sikosehe katika shoo zangu, hivyo mashabiki wangu waendelee kusubiria kazi zangu nyingine ambazo zipo mbioni kutoka" alisema Shilole