Google PlusRSS FeedEmail

WASANII WAMLILIA SHARO MILIONEA


KUTOKANA na kifo cha msanii wa sanaa ya maigizo mwenye staili mpya katika ulimwengu wa comedy Tanzania  ambaye pia aliingia katika fani ya muziki wa kizazi kipya na kupata mafanikio mazuri,Hussein Mkiety Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea baadhi ya wasanii wameeleza hisia zao tofauti kwa  kuguswa na msiba huo

Tasnia ya Sanaa imezidi kukumbwa na jinamizi la kuondokewa na wapendwa wao kwa kipindi cha muda mfupi baada Msanii  na Hussein Mkiety Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea kupata ajali na kufariki jana usiku Barabara ya Segera mkoani  Tanga.

 Kwa mjibu wa rafiki wa karibu wa msanii huyo Ney wa Mitego alisema kuwa marehemu alimuaga anakwenda Tanga kumsalimia mama yake na kupata baraka zaidi baada ya kununua gari jipya ambalo ndilo alipata nalo ajali.

"Kweli siamini macho yangu, nahisi kama ndoto na sasa nipo njiani nakwenda Tanga kwa ajili ya mazishi ya rafiki yangu mpendwa,"alisema

Mwandishi wa habari hii alimtafuta  Mzee Mjuto ambaye alikuwa karibu  na marehemu katika shughuli zao za sanaa hakupatikana, lakini mtoto wa Mzee Majuto Hamza Majuto alibainisha kuwa hali baba yake si nzuri baada ya kupokea taarifa  za kifo hicho juzi usiku na walimpeleka hospitali kwa matibabu zaidi lakini alipata nafuu.

Asubuhi walipanga safari ya kwenda kwenye msiba Mheza lakini hali yake si nzuri kutokana na mshtuko wa taarifa hizo.

"Naomba tumwache baba kwa sasa kwani hawezi kusema lolote , ameshtuka sana na kifo hicho, ndugu mwandishi hapa tupo njiani tunakwenda huko kwa ajili ya mazishi, tutazidi kuwasilina asante," alisema

Wakati huo huo  Hamza alibainisha kuwa wanatarajia kufanya maziko kesho nyumbani kwa wazazi wa marehemu, Muheza saa saba mchana.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii msanii Shilole alisema Sharo alikuwa mtu wake wa karibu hatua ilichangia baadhi ya watu kutilia shaka uhusiano wao kama ni wa  kimapenzi kikazi.

"Kweli mwandishi mimi siamini kama kweli sharo hayupo tena nasi inaniuma sana nashindwa hata kuelezea," alisema huku akiwa na akilia kwa kwikwi na kushindwa kuzungumza vizuri na kuongeza

"Sharo ni mtu wangu wa karibu tayari tulishapanga naye kufanya naye 'singo'  siwezi kusema mengi ila inaniuma sana nahisi kama ni ndoto jamani Sharo kwangu alikuwa ni zaidi ya rafiki hadi watu walikuwa wanahisi nina mahusiano naye ya kimapenzi na nyimbo yake ya kwanza aliniimbia mimi inauma sana,"alisema  Shilole huku akionekana amejaa na majonzi

Wakati huo huo msanii Dully Skykes ambaye pia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya na amabaye amefanya naye kazi ya mwisho inayojulikana kwa jina la 'Chuki ya Bure' alisema kuwa hakuamini baada ya kupokea taarifa hizo za kushtua na kusikitisha kwani walikuwa bado wanandoto kubwa ya kufanya mambo mengi katika tasnia ya muziki

Alisema kuwa mara ya mwisho walizungumza naye siku ya Jumapili huku wakiwa na mikakati ya kufanya kazi ya pamoja ambayo Dully ameiandaa ila sasa ndoto hiyo imezima kama mshumaa.




This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging