MSANII wa muziki wa kizazi kipya kutoka Nyumba ya kukuza Vipaji (THT) Amini Mwinyimkuu a.k.a Amini akiri kutopata msichana mwingine kwa kipindi chote alichoachana na aliyekuwa mpenzi wake ambaye pia ni msanii mwenzie Linah Sanga 'Linah'
Msanii huyo alikiri kuwa aliishi kwa muda wa miaka mitatu na hawajawahi kugombana kwa kipindi chote hicho na wala kufumaniana hali hiyo inaonyesha ni jinsi gani kila mmoja wao alivyokuwa na mapenzi ya ukweli katika mahusiano yao ambapo kwa sasa hayako tena
Amini aliweka wazi hayo jijini Dar es Salaam baada ya kuelezea mahudhui ya nyimbo inayoitwa 'Mtima wangu' aliyoifanya kwa kushirikiana na Linah na mikakati aliyokuwa nayo juu ya utengenezaji bora wa video ya nyimbo hiyo anayotarajia kuitoa mwishoni mwa mwezi huu kama zawadi ya mashabiki wake katika kipindi cha kufunga mwaka
Alisema kuwa kwa kipindi chote hicho ambacho walikuwa na mahusiano na Linah amekuwa mkweli na walikuwa na ndoto nyingi ambazo hazijaweza kutimia kwa kuvunjika kwa mahusiano yao
"Sijawahi kufikiria na bado sijapata mwanamke ambaye anaweza kuziba pengo la Linah kwani yeye alikuwa ni mwanamke wa kipekee kwangu na kwa kipindi chote nilichokaa naye katika mahusiano yeye alikuwa bora kwangu" alisema Amini
Akizungumzia kuhusu kurudiana kwao alisema kuwa ukweli uko moyoni mwao na mapenzi ni kikohozi hivyo kama watakuwa wamerudiana ukweli utafahamika siku moja itakapo fika ingawa kwa sasa hayuko teyari kuzungumzia hilo swala