DR. DRE ATAJWA KUWA MWANAMUZIKI ANAYELIPYWA ZAIDI
Kwa mujibu wa jarida la Forbes mwanamuziki Dr. Dre ndiye mwanamuziki anayelipwa sana kwa mwaka 2012. Dre amejikusanyia kiasi cha US dola milioni 110. "Hivyo ndivyo alivyo." alisema raisi wa zamani wa Def Jam Kevin Liles.
"Kama utaangalia watu ambao wanaongoza kupata pesa nyingi, Dre amekuwa akifanya hivyo kwa miaka 20 sasa. Kinachotokea sasa ni kwamba watu wanasema ukweli." alimalizia kusema raisi huyo wa zamani wa Def Jam
Wasanii wengine ambao wameingia katika orodha ya wasanii wanaoingiza pesa kubwa ni pamoja na Rihanna anayeshika nafasi ya pili akiwa anaingiza US dola milioni 53, Diddy anafungana na Katy Perry katika nafasi ya 15 wakiwa wanaingiza US dola milioni 45. Beyonce anashika nafasi ya 18 akiwa anaingiza US dola milioni 40 huku mme wake Jay-Z akiwa nafasi ya 20 akiingiza US dola milioni 38. Kanye West anashika nafasi ya 22 akifungana na Adele katika nafasi hiyo wakiwa wanaingiza US dola milioni 35.
Orodha ya wasanii wanaoongoza kuingiza pesa nyingi ni hii
1. Dr Dre – $110 Million
2. Roger Waters – $88 Million
3. Elton John – $80 Million
4. U2 – $78 Million
5. Take That – $69 Million
6. Bon Jovi – $60 Million
7. Britney Spears – $58 Million
8. Paul McCartney – $57 Million
8. Taylor Swift – $57 Million
10. Justin Bieber – $55 Million
10. Toby Keith – $55 Million
12. Rihanna – $53 Million
13. Lady GaGa – $52 Million
14. Foo Fighters – $47 Million
15. Diddy – $45 Million
15. Katy Perry – $45 Million
17. Kenny Chesney – $44 Million
18. BeyoncĂ© – $40 Million
19. Red Hot Chili Peppers – $39 Million
20. Jay-Z – $38 Million
21. Coldplay – $37 Million
22. Adele – $35 Million
22. Kanye West – $35 Million
24. Michael BublĂ© – $34 Million
25. Sade – $33 Million