JK AWATUNUKU BI. KIDUDE NA GURUMO
Rais Jakaya Kikwete amewatunuku nishani ya heshima ya Jamhuri ya Muungano wa wanamuziki watatu, msanii mmoja wa maigizo , wasanii wa michezo hao wamepewa tuzo hizo Jana jioni katika hafla iliyofanyika viwanja vya Ikulu Dar es Salaam
Utoaji wa nishani hizo ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam
Wasanii waliopewa nishani hizo ni kiongozi wa dansi ya Msondo Ngoma, Muhidin Gurumo, pia kiongozi wa zamani wa bendi ya Dar es Salaam International, Marijani Rajabu na muimbaji mkongwe wa taarabu Fatuma Baraka 'Bi. Kidude
Wengine ni aliyekuwa msanii maarufu wa maigizo na filamu nchini marehemu Fundi Said ' Mzee Kipa