FILAMU YA KUMSAPOTI JK KUPIMA VVU YAZINDULIWA
Filamu mpya iitwayo 'Shujaa' imezinduliwa kuelezea kisa cha kweli cha mvulana aliyemuokoa msichana asiambukizwe virusi vya ugonjwa wa ukimwi
Utayarishaji wa filamu hiyo unalenga kuunga mkono juhudi za Rais Jakaya Kikwete za kuhamasisha jamii kupima afya na hasa VVU
Adam Kisale ambaye ni mkurugenzi wa filamu hiyo alisema kuwa kitendo cha Rais Kikwete kupima VVU hadharani kiliwatia moyo wengi na hasa vijana wakahamasika kupima afya zao
"Hali hiyo ilifikia watu kuanzisha msemo wa 'Unaringa umepima' hivyo tukachukua jukumu la kuandaa filamu hii ili kuwasilisha ujumbe kwa jamii" alisema Kisale
Alisema kuwa filamu hiyo imeshirikisha wasanii nane wakiongozwa na Irene Paul ambaye ni msanii wa bongo movi pamoja na Henry Babuu, Mashaka, Juma Rajabu, Bandago Mzee Bareshi, Muba na Bi. Salama