Mwanamuziki nguli wa dansi JB Mpiana pamoja na kundi la wenge BCBG waamekonga nyoyo za mashabiki wa muziki wa dansi Dar es Salaam jana katika viwanja vya Leaders Club baada ya kufanya shoo ya nguvu huku akiwapa mashabiki wake vionjo vya nyimbo za zamani
Shoo hiyo ilihudhuriwa na baadhi ya wasanii na waimbaji wa nyimbo za dansi ilionekana kufana zaidi baada ya JB Mpiana kuimba vibao vya kale huku akionekana kuwakumbusha mashabiki wake vionjo hivyo ambavyo vilionekana kupitwa muda wake