Msako wa nyumba hadi nyumba uliofanywa na polisi kwa ushirikiano na wananchi ulifanikisha kupatikana kwa tairi la akiba la gari alilokuwa akiendesha, radio ya gari pamoja na betri ya gari hilo
Msako huo pia ulisababisha kupatikana kwa vitu vingine kama kama simu ya mkononi, saa ya mkononi, na nguo alizokuwa amevaa marehemu
Kusalimishwa kwa vitu hivyo kumetokana na agizo la Mkuu wa wilaya hiyo Bi. Subira Mgalu ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama, kudai watu wote waliomuibia marehemu baada ya ajali watasakwa na kuchukuliwa hatua za kisheria
Sharo Milionea alifariki baada ya gari alilokuwa akiendesha kutoka aina ya Toyota Harrier kupasuka tairi ya mbele akiwa katika mwendo kasi na kupinduka mara kadhaa wakati akitoka Dar es Salaam
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoani humo ACP Constantine Massawe alisema usiku wa kuamkia juzi Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw. Abdi Zawadi alipeleka vifaa mbalimbali vya marehemu