MZEE MAJUTO : "JOTI NDIO MSANII PEKEE ANAYEWEZA KUFANYA KAZI NA MIMI"
Msanii wa vichekesho nchini Mzee Majuto ameendelea kusikitika na kukiri kuwa pengo la aliyekuwa msanii maarufu wa filamu na muziki wa kizazi kipya Tanzania Hussein Ramadhani, 'Sharo Milionea',alizibiki na mtu yeyeto yule ingawa msanii peke kwa sasa aliyebaki ambaye anaweza kufanya naye kazi ni Lukac Mhavile a.k.a Joti wa kundi la Ze Comedy
Aliyasema hayo alipotoka kumzika msanii aliyekuwa anafanya naye kazi Sharo Milionea na kuendelea kusisitiza kuwa baadhi ya wasanii wengi hapa nchini hawana heshima na hawapo kwa ajili ya kufanya kazi
Alisema kuwa marehemu alikuwa na heshima ya kazi na alikuwa anajua anachokitaka na ndio maana aliweza kufanya kazi kwa kipindi chote na kuingia mikataba mbalimbali mpaka umauti ulipomfika
Kwa upande wake msanii wa vichekesho Joti alisema kuwa kuna vitu ambavyo ameviona yeye anavyo vilivyomsababisha mpaka Mzee Majuto kufikiria kuwa anauwezo wa kufanya naye kazi
"Kwanza nashukuru sana kwa mzee huyu kuniona kwani wapo wasanii kibao ambao wamenitangulia mimi kwenye kazi lakini ameniona kuwa ninasifa, naamini kuna vitu ambavyo ninavyo vinavyomvutia mpaka kufikiria kuwa nina kila sababu ya kufanya naye kazi" alisema Joti
Aliendelea kusema kuwa nidhamu ni muhimili mkubwa anaoutumia katika kazi zake ili aendelee kuwa bora, kwani bila ya kuwa na misingi imara ya nidhamu wasanii hawataweza kufika popote wanapotaka
Joti aliongezea kwamba vitu ambavyo mzee ameviona kwake ataendelea kuvidumisha ili kuendelea kuwa kivutio kwa kila mtu