JULIANA KANYOMOZI ASHEREHEKEA KUTIMIZA MIAKA 31
Amefanya muziki kimafanikio tangu mwaka 2000 akiwa katika kundi la I-Jay akiwa na Iryn Namubiru, na hadi sasa wakati akitimiza umri wa miaka 31 Juliana bado anaonekana mrembo na mwenye mvuto
Mwaka huu umekuwa mzuri kwa mama huyo wa mtoto mmoja ambaye anaweza kumaliza mwaka bila ya kutoa 'single' kutokea kushinda tuzo ya BEFFTA (UK) Award kuachia 'single' mpya ya 'Ndibulungi' kupata dili ya kuwa jaji wa shindalo la vipaji vya kuimba la 'Tusker Project Fame hadi kushirikiana na msanii anayetamba nchini Ghana, Jay Ghartey katika wimbo aliouita 'Love you Better' Juliana anatabiliwa kuongoza chati za muziki 2013
"Aina ya sauti ni adimu kuipata kokote ni binti wa kisasa na ni rahisi kufahamu kwa nini watu wanampenda sana Nilijiona mwenye bahati kufanya kazi na mtu mwenye kipaji kama yeye" Jay Ghartye alisema wakati akitoa mtazamo wake kwa Juliana mjini Accra
Akijibu meseji za kumpongeza kwa siku yake ya kuzaliwa katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii Juliana aliandika "Asante kwa upendo huu mnaonionyeshea mmeugusa uvungu wa moyo wangu sasa nafahamu ni namna gani mnanichukulia Hakika nimeliona pendo lenu kwangu mungu awabariki nyote"