TAFITI: LAPTOP HUHARIBU MBEGU ZA KIUME
DAKTARI bingwa wa masuala ya uzazi Sue Kenworthy wa nchini Marekani amebainisha madhara ya laptop kuwa zinaharibu nguvu za kiume kwa wanaume ambao wanaziweka juu ya mapaja.
Aliwashauri wanaume wakati wakitumia Laptop waweke katika meza ili wasiweze kuathiriwa na miozi hiyo.
"Wataalum mbalimbali wamethibitisha kuwa joto linalotolewa na laptop inapotumika ikiwa katika mapaja
huchangia kwa asilimia kubwa kuharibika kwa mbegu za kiume na kushindwa kupata watoto na wake zao.
Utafiti huo pia umethibitishwa na madaktari wa masuala ya uzazi baada ya kupima joto la laptop baada kukutana na kesi nyingi za wanaume kukosa watoto na walipopimwa waligundulika kuwa mbegu zao zimeharibika kutokana na joto la laptop.
Hapo awali wanaume wengi walikuwa wanafikiri kuwa wanawake wao ndio wana matatizo kumbe sivyo kwani wapo wanaume ambao mbegu zao zinahariba bila wao kujua.
Madktari walibainisha ushuhuda wa kijana moja mbaye walimshauriwa ache kutumia laptop katika mapaja yake na atapata mtoto, kweli alivyofanya hivyo kwa muda wa miezi mitatu mke wake alipata mimba.
Kijana huyo alikuwa akiitumia laptop yake kila siku jioni kwa saa kadhaa akiwa ameiweka mapajani na alikuwa hana elimu kuwa laptop ina madhara kiasi hicho.