KATY ACHAGULIWA MWANAMKE BORA WA BILLBOARD
MWIMBAJI Katy Perry amechaguliwa kuwa mwanamke bora wa mwaka wa Billoard, chati inayoongoza
dunia.Lakini Katy amedai kuwa mafanikio hayo yametokana na kazi nzuri aliyoifanya mwaka jana.
"Kama ni mwaka ambao nitaupenda ni mwaka jana, mambo yangu mengi yalikwenda", alisema alipohojiwa na mtangazaji wa Billboard, Jon Stewart.
Perry aliachia albamu ya "Teenage Dream" mwaka 2010, na nyimbo zake tano kushika nafasi tano za juu katika chati hizo za Billboard Hot 100.Katy ambaye pia ni mwanamitindo na mtunzi wa nyimbo alidai kuwa anataka kuonekana kama kioo kwa mabinti wadogo kutokana na mafanikio anayopata.