BABY MADAHA AJIVUNIA KUTUNGA MISTARI AKIWA MTUPU
MSANII wa kike anayetamba kwenye gemu la muziki wa bongo fleva Baby Madaha anajikuta nafungua mwaka na kituko cha aina yake kwa kupenda kukaa utupu bila ya kuvaa chochote pindi awapo nyumbani kwake
Nyota huyo ambaye anajikuta kupenda kukaa utupu siku nzima awapo nyumbani kwake bila ya kuvaa nguo yoyote ile hali hiyo inampa ugumu sana pindi anapotembelewa na wageni nyumbani kwake
Mwenyewe anabainisha kuwa anapata mawazo ya nyimbo mpya akiwa na hali hiyo ya kutovaa nguo, na kuweza kuandika mistari ya nyimbo akiwa katika hali ya utupu
Akiwa bafuni pia ndio muda wake mzuri kwake wa kuendelea kushuka mistari, hivyo bafuni huko anakutumia kwa ajili ya kuogoa na kutunga mistari yake kadhaa ya nyimbo zake
"Ninapenda sana kukaa uchi huku nikiwa naandika mistari ya nyimbo pia ninapokuwa bafuni ndipo muda wangu wa kushuka mistari yaani hali ya kukaa utupu ndio inanisababisha niweze kutunga mistari kwa wingi" alisema Baby Madaha
Hicho ndio kituko cha Baby Madaha ambaye anajikuta akitunga mistari akiwa bafuni huku hali ya kukaa utupu ikimwezesha kupata kilicho bora zaidi katika muziki wake