RIHANNA ATUMIA AKAUNTI YA TWITTER KUTANGAZA NYIMBO YAKE MPYA
Mwanamuziki Rihanna ameamua kuvunja ukimya wake katika matumizi ya akaunti yake ya twitter baada ya hivi karibuni kutumia akaunti yake hiyo na kuitangaza nyimbo yake mpya inayoitwa 'Stay' inayopatikana katika albamu yake ya saba aliyoipa jina la 'UNAPOLOGETIC' huku akisema kuwa amepanga kuachia video ya wimbo wake 'POUR IT UP'
Rihanna alikuwa hajaitumia akaunti yake hiyo ya twitter kwa siku za hivi karibuni ambayo ina watu milioni 27.7 wanaomfuatilia. Lakini mwanamuziki huyo ameamua kuvunja ukimya huo baada ya kuutambulisha wimbo wake mpya 'Stay' uliopo katika albamu yake hiyo mpya . Katika nyimbo hiyo, Rihanna amemshirikisha mwanamuziki Mikky Ekko.