Google PlusRSS FeedEmail

MBUNGE WA KINONDONI KUISAIDIA FAMILIA YA SAJUKI



Kutokana na hali ya majonzi na masikitiko makubwa kwenye familia ya  marehemu Sajuki mbunge wa Kinondoni Iddi Azam ameahidi kuisaidia kwa hali na mali familia aliyoiacha marehemu Sajuki

Ahadi hizo alizisema jana wakati alipofika nyumbani kwa marehemu kwa lengo la kutoa pole na salamu za rambirambi kwenye familia hiyo

Azam alisema kuwa anadeni kubwa kwenye familia hiyo pamoja na  mtoto aliyeachwa na marehemu, hivyo ni wajibu wake kumsaidia kadri ya uwezo wake

"Kila mtu anaiona hali ya Wastara sasa ilivyo basi sisi tulio baki tuwe kama Sajuki, kwani mapenzi walio kuwa nayo ni mfano wa kuigwa kwetu, hivyo nina jukumu la kuisaidia familia hii" alisema Azam

Aliongezea kuwa ni jukumu la kila mmoja wao kumuenzi marehemu Sajuki kwa vitendo Sajuki anazikwa leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam

This entry was posted in

One Response so far.

  1. Anonymous says:

    ashamtamani mtu hapo!

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging