PROFILE : PRODUCER C9
Jina lako halisi ?
C9: Jina nililopewa na wazazi wangu ni Charles Francis, ila jina la kazi naitwa C9 na ndilo lililozoeleka
Wewe ni mtoto wa ngapi kuzaliwa?
C9 : Mimi ni mtoto wa mwisho kati ya watoto watatu
Kabila gani ?
C9 : Mimi ni mngoni kwetu Songea
Elimu yako
C9 : Nimeishia kidato cha sita baada hapo nikaingia chuo kilichopo Zanzibar kwa ajili ya kusomea maswala ya muziki
Kazi ya Producer uliianza lini?
C9 : Kazi hii niliianza mwaka 2004, huku nikiwa nimesoma maswala ya muziki Zanzibar, ambapo nilikuwa na ndoto lukuki za kukuza muziki wa kizazi kipya nchini
kitu gani kilikusababisha ukaingia katika upande wa utengenezaji wa muziki?
C9 : kwa sababu napenda sana muziki na nilikuwa napenda kuimba hiyo ndiyo sababu kubwa iliyonifanya niingie kwenye muziki ingawa hapo awali nilikuwa naimba
Sababu ipi ilikufanya uachane na uimbaji?
C9 : Mwalimu wangu ndiye aliyenishawishi nihamie upande wa utengenezaji wa muziki kwa sababu alikuwa ameona uwezo wangu ulikuwa ni mkubwa mno kwenye utengenezaji wa muziki kuliko kuimba
Changamoto gani unakumbana nazo katika kazi zako?
C9 : Da changamoto kubwa ambayo nakutana nayo ni pale msanii mkubwa yaani mwenye jina anapokuja studio kurekodi ngoma yake bila malipo yoyote wakati msanii chipukizi anakuwa na uwezo wa kulipia ngoma kwa bei kubwa ila yeye mkubwa anakuwa anazingua hiyo inasumbua sana tena muda mwingine inahalibu hadi uhusiano
Nyimbo ambazo zimekutambulisha kwenye gemu ni zipi?
C9 : One love ya Steven, Mama Ntilie hizi ni baadhi ya nyimbo ambazo zilinifanya nijulikane pamoja na kazi zangu kutambulika kijamii
Nyimbo gani ilikuwa ugumu sana studio?
C9 : Nyimbo iliyonipa ugumu ni Bao la Kete nyimbo ya AT kwa sababu kiwango alichokuwa anataka kufika ilikuwa bado sana na yeye alikuwa bado hajatambua nini afanya hilo ndilo lilikuwa ni tatizo kubwa
Ilikuchukua muda gani kuikamilisha nyimbo hiyo
C9 : ilinichukua muda wa wiki tatu kuikamilisha nyimbo hiyo kitu ambacho si cha kawaida sana kwa utengenezaji wa nyimbo
Msanii gani ambaye unatamani kufanya naye kazi?
C9 : Natamani sana kufanya kazi na msanii Lady Jaydee kwa sababu anajua nini anafanya na anathamini kazi pamoja na nidhamu ya kazi anayo
Unajisikiaje unapotengeneza nyimbo alafu DJ wa redio anasema nyimbo haina kiwango ?
C9 : Huwa nawashangaa madj wa bongo kwani yeye hajui muziki ila anajidai anajua mimi ndiye ninayetengeneza muziki najua nataka utoke kwa kiwango gani yeye anavyoukataa namshangaa na wao ndio wanaoudidimiza muziki wetu