TAFF YATOA ONYO KALI KWA WASANII
Kutokana na kujitokeza kwa utomvu wa nidhamu kwa baadhi ya wasanii wa filamu nchini Shirikisho la Filamu nchini Tanzania (TAFF) limekemea vikali kwa wasanii watakao onyesha utomvu wa nidhamu katika msiba wa Juma Kilowoko 'Sajuki', aliyefariki duniani juzi katika hospitali ya Taifa Muhimbili
Baadhi ya vitendo vya utomvu wa nidhamu ni pamoja na kunywa pombe karibu na maeneo ya msiba huo
Akizungumza nyumbani kwa marehemu Rais wa Shilikisho hilo Simon Mwakifwamba alisema ameshangazwa na kitendo cha baadhi ya wasanii kuacha msiba na kwenda kunywa pombe
Alisema kuwa yeyeto atakaye bainika kufanya vitendo vya utomvu wa nidhamu atachukuliwa hatua kali ikiwemo kumsimamisha kufanya kazi za sanaa
kweli presidaa wajibisha kila mtu atakayekiuka