Google PlusRSS FeedEmail

DIAMOND PLATINUM APORWA CHENI YA GRAMU 25 KWENYE FUJO ILIYOTOKEA KWENYE SHOO YA USIKU WA WASAFII


Msanii anayetamba kwenye tasnia ya  muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul 'Diamond Platinum' amejikuta akianza mwaka vibaya kwa kurushiwa chupa, makopo, maya viza,  pamoja na viti kwenye shoo iliyokuwa ikijulikana Usiku wa Wasafi aliyoifanya  siku ya mwaka mpya Maisha Club jijini Dar es Salaam

Chanzo cha karibu kilieleza kuwa, chanzo cha ugomvi huo umesababishwa na kundi la watoto wa kariakoo ambapo pia ni mashabiki na wadau wa muziki wa kizazi kipya, ambapo makundi hayo huwa yanatumika na baadhi ya wasanii kwa ajili ya kufanya shangwe pale msanii anapofanya shoo ili ionekane shoo hiyo ni kubwa na kujaa watu wengi

Chanzo cha habari kilieleza kuwa Kuna kundi la watoto wa kariakoo ambao walifika Maisha Club kwa ajili ya kumfanyia fujo msanii huyo kwa madai kwamba sasa amebadilika kwa kuwaletea mapozi wenzake hao huku kuonekana kusahau  alipotoka

"Tatizo la Diamond tangu amepata umaarufu amebadilika sana anajikuta anajina kubwa na kusahau alipotoka akipigiwa simu hapokei dharau nyingi sana " kilieleza chanzo hicho

Akizungumza jijini Dar es Salaam Diamond alielezea chanzo cha ugomvi huo ni kutokana na makundi mawili ambayo yapo Kariakoo jijini Dar es Salaam, huku akidai kuwa yeye anamahusiano na mazuri na makundi yote mawili ingawa makundi hayo hayana maelewao mazuri wenyewe kwa wenyewe

"Mimi ni mtoto wa Kariakoo hivyo kuna makundi mawili moja linajiita Hela na lingine linajiita Hela kujinafasi makundi hayo hawaelewani ingawa mimi nina ongea nao wote kwa hiyo hilo ni tatizo kwa kutokana na kuwa na mvutano wa pande mbili kila upande mmoja hautaki mimi nizungumze na kundi lingine wakati kwa muda huu si vizuri mimi kujigawa kwenye makundi" alisema Diamond

Alisema kuwa alipata taarifa za fujo kabla ya yeye kupanda kwenye shoo hiyo na alichukua hatua kwa kutoa taarifa kwa uongozi juu ya watu kuhisiwa kutaka kufanya fujo kwenye shoo hiyo

Pamoja na hayo diamond alisema kuwa kwenye fujo hizo aliporwa vitu vyake vya thamani cheni ya gramu 25, pete pamoja na saa ya mkononi

Aliongeza kuwa ameshatoa taarifa polisi juu ya fujo hizo na kuahidi kuwa watu hao watakapokamatwa lazima waombe msamaha kwa mashabiki wake kwenye vyombo vya habari

Fujo hizo zilitokea jana kwenye shoo ya Usiku wa Wasafi

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging