JOKETI AJIPANGA KUSAIDIA WATOTO WAKIKE
ALIYEKUWA miss Tanzania 2006 Joketi Mwegelo aanza kusaidia watoto wa kike waliopo mashuleni kwa ajili ya kukuza uelewa pamoja na vipaji walivyonavyo ili viweze kuwasaidia katika kupata maendeleo kwa jamii inayowazunguka pamoja na kutimiza malengo waliojiwekea
Akizungumza jijini Dar es Salaam alisema kuwa ameandaa mpango maalumu kwa ajili ya kutembelea mashuleni ambapo anatarajia kuanza mikoa ya kaskazini ili aweze kutimiza lengo lake la kuwasaidia watoto wa kike wenye vipaji mbalimbali
Kutokana na hilo aliweka wazi kuwa atatumia muda wa ziada kwa ajili ya kuwajenga watoto wa kike kuelewa umuhimu wa elimu na jinsi ya kuifanyia kazi bila ya kutegemea kuajiliwa
"Ili msichana aweze kufika pale anapohitaji yeye lazima apate msaada wa kujengwa kifira na akili hivyo nachukua nafasi yangu kwa ajili ya kuwajenga wasichana kwani naamini unapomsaidia mtoto wa kike ndipo umeweza kusaidia taifa kwa ujumla" alisema Joketi
Mbali na hayo alitoa wito kwa watu maarufu kutumia elimu na hata wengine kujiendeleza kielimu kwani elimu ni muhimili katika maisha na inasaidia kukuza fikira na kufanya maamuzi yaliyo sahihi
Joketi ambaye kwa sasa amejikita katika maswala ya ujasiriamali ambapo teyari ameweza kuingiza sokoni nywele zake zenye nembo ya kidoti huku akionyesha kuwajali wasichana pamoja na kinamama wanaopenda urembo kwa kuingiza sokoni nywele yenye ubora wa hali ya juu