MAUZO WA EXTRA BONGO APANIA KUFANYA KWELI
MUIMBAJI wa nyimbo za bendi kutoka Extra Bongo wazee wa 'kizigo' Redock Mauzo apania kuleta mabadiliko ikiwemo kuwa mbunifu katika tungo zake pamoja na kazi zake anazozifanya ikiwa kama mchango wa kuendelea kukuza na kuifikisha mbali bendi hiyo
Akizungumza katika onyesho la bonanza la kila jumapili alisema kuwa aliingia na bendi hiyo kutokana na kipaji alichonacho hivyo anaamini kuwa atafanya vizuri na kuhakikisha mafanikio yanapatikana katika bendi hiyo ili aweze kujitangaza zaidi katika kazi anazozifanya
Alisema kuwa baadhi ya wanamuziki wanaonekana kuyumba kwa kukosa ubunifu na uwezo wa kujitofautisha na waimbaji wengine hivyo ili uweze kufika mbali ubunifu na kujitofautisha ndio msingi wa muziki wa hapa nchini
"Katika kazi ya uimbaji lazima uwe tofauti lakini mnapoigana na kuwa na kitu kimoja hali inayoonyesha kushindwa kufanya kazi ya uimbaji na kupoteza radha hiyo hivyo ili uweze kubaki kileleni lazima uwe tofauti na waimbaji wengine"
Pamoja na hayo alisema kuwa ili kuonyesha yuko tofauti na waimbaji wengine ameweka wazi kuwa anauwezo wa kuimba pamoja na kucheza hali inayomsababisha kuwa na ongezeko la mashabiki wengi
Aliongezea kuwa yeye ni raia wa Kongo hivyo amekuja nchini kwa ajili ya kazi ya muziki kwa hiyo akili yake na uwezo wake wote ameuelekeza kwenye kazi hiyo ili asiwaangushe mashabiki wake ambao teyari ameshajenga uaminifu kutoka kwake