KILA SIKU NI SIKU YA WANAWAKE - SEPETU
WAKATI wanawake wote duniani kusherehekea siku ya wanawake ya tarehe 8 march hali imekuwa tofauti kwa msanii wa filamu nchini Wema Sepetu ambaye husherehekea siku hiyo kila siku kwa kufanya vitu vyenye tija katika jamii vitakavyoweza kumkomboa mwanamke
Wema ambaye huamini siku ya wanawake inatakiwa ienziwe kwa vitendo kila siku ila mtoto wa kike aweze kukombolewa na kupinga vitendo vyote vya ukatili vinavyomdidimiza mwanamke
Hayo yalibainishwa na meneja wake Martini Kadinda jijini Dar es Salaam wakati akielezea mikakati ya kampuni inayomilikiwa na msanii huyo inayojulikana kwa jina ka Endless Fame Films alisema kuwa ili kudhihirisha msanii huyo anawajali na kuwathamini wanawake ametoa kipaumbele kwa kutoa nafasi tatu za ajira kwa ajili ya kuwasaidia wasichana
Alisema kuwa ili waweze kufikia malengo na mafanikio yao wanaamini ubora na usawa ndio ndilo jambo ambalo linaweza kuwafikisha katika malengo hivyo hata watu ambao wapo hufika officini hapo kwa ajili ya usaili huzingatia vitu hivyo
Alisema kuwa ingawa wanazingatia hayo lakini wametoa kipaumbele kwa wasichana ambao pia wanaweza kufanya kazi zinazoweza kufanywa na wanaume hali ambayo pia inajenga hali ya kujiamini kwa mtoto wa kike
"Wema anasaidia sana watoto wa kike ila huwa hapendi kusema amempa huyu nini na yule kipi kwani anaamini kumsaidia mtu si lazima mkono mwingine ujuwe" alisema Martini
Aliongezea kuwa ili kujenga uaminifu na ufanisi sehemu za kazi amepiga marufuku mahusiano ya kimapenzi yenye lengo la kuvunja na kuharibu kazi ndani ya offisi yake, hivyo akibaini hali hiyo atachukua hatua za haraka kuwasimamisha watendaji hao ili wasiharibu jina la offisi yake nje
Pamoja na hayo Martini alitoa wito kwa wasichana wanaotaka kujiunga na maswala ya filamu kuwa wasitumie miili yao kwa ajili ya kupata nafasi ya kuigiza bali watumie kipaji na ubunifu zaidi