Google PlusRSS FeedEmail

NDAUKA AJIPANGA KUWAINUA WATOTO WA KIKE




MAISHA yana changamoto kubwa na ili uweze kuvuka vikwazo na changamoto hizo lazima uwe na mipango endelevu na mikakati iliyothabiti huku ukitimiza ndoto zako huo ni msemo anaotumia msanii wa filamu Tanzania Rose Ndauka alipokutana na mwandishi wa habari hii wiki hii

Mbali na kuwa msanii wa filamu pia ni mwanamke mjasiliamali anayeendesha biashara zake kwa mfumo rasmi huku akiwa ametoa ajira kwa vijana wenzake hususani watoto wa kike

Alianza kujihusisha na maswala ya ujasiliamali mwaka 2011 kwa kufungua kampuni yake inayojulikana kwa jina la ' Ndauka Enterteinment' yenye lengo la kufanya shughuri za burudani, kuandaa matamasha na maswala ya uandaaji wa filamu pamoja na kutoa mafunzo ya filamu kwa vijana chipukizi

Aliamua kujihusisha na maswala ya ujasiliamali baada ya kuona anauwitaji wa kutoa ajira kwa vijana wenzake hususani mtoto wa kike kwani aliamini kuwa ili uweze kukomboa jamii lazima umsaidie mtoto wa kike

Ndauka ameamua kusimamia kazi zake mwenyewe kwa kuindesha kampuni yake ambayo inajihusisha na maswala ya kuandaa matamasha mbalimbali huku akipata muongozo kwa watu wa karibu wanaomzunguka ameweza kutoa ajira kwa vijana wapatao 16, ambao wengi wao ni wasichana

"Niliamua kufungua kampuni yangu mwenyeye kwanza kwa sababu ya kupenda  kuwa mjasiliamali , pili nilitamani kufanya kitu cha tofauti na filamu ili niweze kujiongezea kipato na kuendesha maisha yangu" aliongezea kuwa

"Pia nimevutika zaidi kuwasaidia watoto wa kike kwani naamini endapo unamsaidia mwanamke utakomboa jamii kwa ujumla na kukuza uchumi wa nchi hii ndiyo sababu iliyonipelekea kufanya hivyo" alisema Rose

Kwa upande wa filamu Rose alianza kujiingiza kwenye filamu mwaka 2005, kwa msaada wa msanii mwenzie Rich Rich ambaye ndiye aliyemvuta katika fani hiyo

Aliweza kuonekana kwenye filamu mbalimbali ambazo alishirikishwa na wasanii wenzie huku akionekana mahiri kwa kuweza kucheza nafasi alizopewa kwa kuvaa uhusika vilivyo

Rose pia aliweza kuonekana kwenye filamu tofauti tofauti kama 'Cut Off' aliyocheza pamoja na wasanii wenzie Cheki Budi, Cloud aliweza kuonekana mahiri zaidi kwa kuvaa uhusika na kuthibitisha kuwa na kipaji cha uigizaji

Mwaka 2010 aliweza kuanza kufanya kazi zake mwenyewe kwa kuandika story pamoja na kufanya maandalizi ya filamu bila ya kumtegemea mtu hali iliyosababisha kuzidi kujiimarisha katika upande wa filamu

Alifanikiwa kuingiza sokoni filamu inayojulikana kwa jina la 'The Diary' ambayo yeye ndiye alikuwa mwandishi wa wa filamu hiyo iliyochezwa na wadada watatu akiwemo Wema Sepetu na Jaqrine Pentezely

Mwanadada huyo kwa kuonyesha nia ya dhati ya kufikisha filamu za Tanzania katika ngazi ya kimataifa ameweza kufanya uzinduzi wa filamu yake inayojulikana kwa jina la 'Waiting Soul' jijini Mbeya mwaka huu

Mwanadada huyo ambaye ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto watatu, anaelimu ya kidato cha nne amejiingiza katika tasnia ya filamu kwa sababu anaamini kuwa anakipaji na uwezo wa kuelimisha jamii kupitia kipaji hicho

Anapenda mavazi yenye mchanganyiko wa rangi huku rangi nyekundu na nyeusi akiipa kipaumbele, ingawa anazingatia ubunifu katika uvaaji wake na kuwapa ushirikiano wabunifu wa nyumbani

Siku za mapumziko anapenda kukaa sehemu za ufukwe huku akipendelea kunywa juice ikiwa ni sehemu ya kinywaji chake ,na kuangalia sinema sehemu mbalimbali ingawa anatumia muda wa ziada kusoma vitabu na kuongea na marafiki wanaomtembelea nyumbani kwake



Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging