Google PlusRSS FeedEmail

LADY JAYDEE ATOA SHAVU KWA MASHABIKI WAKE



MSANII mkongwe wa muziki nchini Lady Jaydee aonyesha kuwajali mashabiki wake kwa kutoa saa moja kwa mashabiki wake kumuuliza swali lolote la msingi

Alitoa nafasi hiyo kwa kupitia mtandao wa kijamii 'Facebook' kwa kuwapa mashabiki wake nafasi ya kumuuliza chochote kile ingawa alitoa angalizo kuwa maswahili yote atakayoulizwa yawe ya msingi na kufuata maadili

"Muda huu niko free ku chat hapa, nina kama saa moja tu nzima.
Karibuni sana, Una swali? Jitahidi liwe la msingi." ndio ujumbe alioutuma kwenye ukurasa wake wa Facebook ili kutoa nafasi kwa mashabiki wake kumuuliza maswali ya msingi

Mashabiki wake wapatao 173 walimuuliza maswali mbalimbali ingwa baadhi ya mashabiki wengi wamempongeza kuendelea kuwepo kwenye gemu la muziki kwa muda mrefu huku akiendelea kuwa na heshima pamoja na kumuheshimu mumewake huku akionekana ni msanii wa pekee aliyeweza kudumu kwenye ndoa yake

Mmoja wa shabiki wake aliyejulikana kwa jina la Emmanuel Mtey aliandika hivi kwenye ukurasa huo wa facebook "Nakupenda na ninaupenda uhusiano wako, uko vizuri sana kwanza una kipaji unajiheshimu ni mwanamke wa kuigwa"

Jaydee aliweza kuyajibu maswali mengi ambayo yalikuwa yakiulizwa na mashabiki wake huku maswali hayo yalijaa pongezi na baadhi yalikuwa yanauliza juu ya ujio wa albamu yake inayojulikana kwa jina la Joto Hasira

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging