Google PlusRSS FeedEmail

JAYDEE ATINGA MAHAKAMANI



MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura 'Lady Jaydee' 'Anakonda' jana amefika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa ajili ya kupokea barua ya kumtaka afike mahakamani Mei 27, mwaka huu.

Barua hiyo inamtaka msanii huyo kwenda mahakamani hapo kutokana na kesi ya madai, iliyofunguliwa dhidi yake ambapo kesi hiyo ipo chini ya Hakimu Athuman Nyamlani.

Msanii huyo amefunguliwa kesi hiyo ya madai na Mkurugenzi wa Clouds Media, Joseph Kusaga pamoja.

Akizungumza nje ya mahakama hiyo na waandishi wa habari mahakamani hapo, Jaydee alisema barua hiyo inamtaka afike tarehe hiyo kwa ajili ya usikilizwaji wa shauri linalomkabili.

Alisema kwa mujibu wa barua hiyo inaonesha kesi hiyo ya madai amefunguliwa na Kusaga na Mkurugenzi mwenzake Ruge Mutahaba.

Hata hivyo, Jaydee hakuwa tayari kuzungumzia kesi hiyo kiundani na kudai mpaka atakapowasiliana na mwanasheria wake.

Jaydee na Clouds waliingia katika malumbano kwa muda mrefu ambapo msanii huyo alikuwa akilalamika kubaniwa nyimbo zake kupigwa katika kituo cha redio cha Clouds, ambacho kipo chini ya wakurugenzi hao.

Pia msanii huyo alikuwa akilalamika kuwa kituo hicho redio kimeshindwa kupiga matangazo yake licha ya kwamba alilipia.




This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging