Gillie pia najaipanga kucheza kama staring kwenye filamu mpya ya Suge Knight. Katika filamu hiyo, msanii huyo rapa wa Philladelphia nchini Marekani atacheza kama Tupac Shakur.
“Ni dhahiri kwamba tunayo bajet tayari, hivyo nasubir kujua ni lini tunaanza kurekodi” Gillie aliuambia mtandao mmoja maarufu wa AllHiphop.com, “mimi sio mwongozaji katika filamu hiyo bali ni mcheza filamu tu. Nikiambiwa muda wa kuchapa kazi umefika, naingia kazini, kila kitu kipo tayari” alisema Gillie