Kutokana na kitendo chake cha kuchelewa mara kwa mara kwenye shoo mwanadada Rihanna ajikuta yupo katika wakati mguu baada ya mashabiki kumwagia chipsi.
Mashabiki hao walionyesha kuchoshwa na tabia yake ya kuchelewa ovyo kwenye maonyesho yake,safari hii mashabiki hao walionekana kujipanga ili kuikomesha tabia hiyo ya mwanadada huyo kwa kumwagia chips jukwwani baada ya kuchelewa kufika katika onesho lake la Diamonds huko Manchester, Uingereza . onyesho hilo lilifanyika siku ya Jumanne wiki hii.
Kutokana na kitendo hiko kilikuwa cha ghafla mwanadada huyo hakufikilia kutumia njia ya haraka hata kuchukua mwamvuli wake maarufu 'Umbrella' kujikinga na chips hizo kutoka kwa mashabiki hao ambao pamoja na hasira lakini bado walimngoja kwa hamu.
Rihanna alichelewa kwa saa moja, lakini kitendo hiko si cha mara ya kwanza kuchelewa katika matamasha yake hali inayopandisha hasira kwa mashabiki wake wanaofika kwa wingi kumuona.
Mwezi march mwaka huu alichelewa masaa 2 katika onyesho la Montreal, July 6 alichelewa tena masawa mawili huku akiwa amelewa chakali.
Rihanna baada ya kumwagiwa chipsi hizo jukwaani kutoka kwa mashabiki wake alijikuta akijibu mashambulizi hayo kwa kutoa maneno makali