Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Kala Jeremiah awataka mashabiki wake kujiandaa kuipokea ngoma mpya ambayo anatarajia kuiachia hivi karibuni.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Kala aliweka wazi kuwa baada ya mfungo wa mwenzi mtukufu wa ramadhani anatarajia kuachia nyimbo mpya ambayo itaendana na mazingira ya kipindi hicho.
Kala ambaye amenyakua tuzo tatu za Tanzania Kilimanjaro Music Awards, huku akiibuka kidedea kwenye upande wa mwanamuziki bora wa Hip Hop, aliweka wazi kuwa sasa yupo katika maandalizi ya mwisho ya nyimbo hiyo ambayo hakutaka kuweka wazi jina la nyimbo hilo.