Google PlusRSS FeedEmail

KUNDI LA CHEMBA SQUAD HALIJAWAHI KUVUNJIKA , WAJIPANGA KUTOA NYIMBO YA KUMUENZI NGWAIR


MUZIKI wa kizazi kipya  ni moja ya fani inayokuwa kila siku huku ikiongeza idadi ya vijana wengi kuingia katika fani hiyo, ambayo imetoa ajira kwa vijana wengi nchini huku wengine wakiendesha maisha yao kupitia muziki huo.

Kipindi cha miaka ya 2000 ndani ya muziki wa bongo fleva, kuliibuka makundi mbalimbali ya muziki nchini yenye lengo la kuburudisha kuelimisha ikiwemo kuleta umoja unaonganishwa na vijana hao kwa njia ya muziki.

Kundi  la Chemba Squad ni miongoni mwa makundi machache ya kitambo ambayo bado yanafanya kweli katika ulimwengu wa muziki wa Bongo Fleva, ingawa kwa kipindi hiki kumekuwa na ukimya wa aina yake.

Ukizungumzia kundi hilo bila shaka utamzungumzia msanii Moses Bushagama 'Mez B' ambaye ni miongoni mwa wasanii wanaounda kundi hilo lenye makao makuu yake  mjini Dodoma.

Kabla ya kuunda kundi hilo msanii huyo waliunda kundi lililokuwa likijulikana kwa jina la 'Chemba Fleva Guyz' ambapo kundi hilo liliundwa na wasanii watatu.

Kundi hilo ambalo liliundwa na Mez B mwenyewe marehemu 'Mang Air' Ngwair pamoja na Mallo Star ambaye sasa ameacha muziki.

Baada ya kujiunga na shule ya Sekondari Mazengo mkoani Dodoma ndipo walipojikuta wakiungana na baadhi ya wasanii wengine akiwemo Dark Master, marehemu Ngwair.

Kundi hilo liliundwa na wakali kama Ngwair,Noorah, Dark Master pamoja na Mez B  ambao kila mmoja akiwa na ndoto ya kuwa msanii wa kimataifa huku wakiutangaza vyema muziki ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Baada ya kumpoteza msanii mwenzao Ngwair wanachemba Squad wajipanga kutoa nyimbo maalumu ya kumuenzi msanii huyo itakayoitwa 'nina imani' ambayo ni maalumu kwa ajili ya kumuenzi msanii huyo.

Neno la Chemba Squad lilitokana na vyumba walivyokuwa wanatumia kwa ajili ya kusomea, ambapo hivyo vyumba ndivyo vilivyozalisha jina la kundi hilo.

Kundi hilo ni kundi la kipekee ambalo halijawahi kuvunjika, ukitofautisha na makundi ya baadhi ya wasanii wengine wa muziki wa kizazi kipya ambayo huvunjika kwa kipindi kifupu kutokana na sababu mbalimbali.

Mez B anajivunia kuwa kwenye kundi ambalo ni miongoni mwa kundi la kipekee lililodumu ndani ya muziki huo, ingawa hivi sasa wamempoteza mmoja wa wao ambaye ni marehemu Albert Mangwea hivi karibuni.

Mez B ni miongoni mwa wasanii walioanza kuwika kwenye gemu mnamo miaka ya 2000, ingawa alianza muziki akiwa yupo masomoni, huku akiamini kuna siku atakuwa msanii wa kimataifa.

Msanii huyu ambaye anafanya miondoko ya R&B huku akiwa ameshawahi kutamba katika gemu hilo kwa kipindi hicho kutokana na nyimbo zake zilizowahi kubamba kwa miaka hiyo.

Mbali na kuwa na uwezo wa kufanya miondoko hiyo pia anauwezo wa kufanya muziki ya miondoko mbalimbali ikiwemo kwaito, zuku rhumba ingawa amejikita kwenye muziki wa aina hiyo .

Kutokana na ndoto zake za kuwa msanii bora Mez B alifanikiwa kutoa nyimbo mbalimbali zilizomtambulisha vyema huku baadhi ya nyimbo akiwa ameshirikiana na baadhi ya wasanii wa muziki huo akiwemo Ray C.

Mez B aliweza kutambulika kwa ngoma 'Kikuku cha Mama roda, 'Kama Vipi', ambayo alishirikiana na msanii Ray C.

Mez B ni miongoni mwa wasanii waliokumbwa na changamoto kubwa ndani ya tasnia ya sanaa, ambapo anaamini baadhi ya wasanii wanaopata majini hawatendei haki tasnia hiyo kutokana na tungo zao kukosa ubora.

Akizungumza na mwandishi wa makala hii msanii huyo aliweka wazi kuwa kuna tofauti kubwa muziki wa kipindi hiki na ule wa zamani huku akiweka wazi muziki wa sasa umejaa kuigana na kukosa ubora kwenye jamii

Alisema hali hiyo inasababishwa na baadhi ya wasanii kukosa tungo zenye ubora pamoja na kuishia kutunga vitu ambavyo havina ujumbe sahihi kwa jamii.

Mbali na hiyo aliweka wazi ili muziki uwende kimataifa inapaswa muziki huo kubadilika pamoja na baadhi ya wasanii huku wakitambua soko la kimataifa linataka kitu gani.

Mez B ambaye anajipanga kurudi tena kwenye gemu la muziki, huku akiamini kuwa atakuja kubadilisha mtazamo wa muziki huyo na kuwateka upywa mashabiki wake ambao hawajamsikia kwa muda mrefu.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging