MEZ B NA MIKAKATI YA NDOA
BAADA ya baadhi ya washabiki wa muziki wa bongo fleva nchi kujiuuliza maswali mengi juu ya baadhi ya wasanii kushindwa kuoa pamoja na kupata watoto, msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Moses Bushagama 'Mez B' ameweka wazi sababu zinazopelekea baadhi ya wasanii hao kushindwa kuoa.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii, msanii huyo alisema kuwa mazingira wanayoishi ni miongoni mwa sababu inayopelekea kushindwa kupata mwanamke sahihi wa kutengeneza naye maisha.
Alisema kuwa baadhi ya wasichana wanajiingiza mahusiano na baadhi ya wasanii siyo kwa mapenzi ya dhati bali ni kwa kupenda nyimbo yake fulani, na inapofika msanii mwingine katoa nyimbo nyingine kali anaachana naye na anahamia kwa hhuyu mwingine.
Aliendelea kuelezea kuwa baadhi wasichana wengine ambao wanakuwa na mapenzi ya dhati wanaogopa kuwakubali wasanii hao kwa kudhani kuwa ni wahuni.
Kutokana na hilo aliongezea kuwa inawawia ugumu kupata chaguo sahihi kwani kuoa ni suala la makubaliano yanayofanywa na pande zote mbili pamoja na kushirikisha wazazi.