Google PlusRSS FeedEmail

NEY WA MITEGO ALIZWA NA HALI NGUMU YA AKINA MAMA


MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Ney wa Mitego amejikuta akitokwa na machozi, baada ya kukutana na mwanamke akiwa amewabeba watoto wawili wadogo huku akiendesha baiskeli mkoani Morogoro wilayani Ifakara.

Hali ilimkuta baada ya kumuona mama huyo, akiwa ametoka shamba akiwa amewabeba watoto wake wa kike wadogo, huku akiwa anaendesha baiskeli hiyo na ndoo ikiwa imening'inia mbele.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi msanii huyo alisema wazi kuwa ugumu wa maisha, unawaumiza wanawake na watoto wadogo ambao mara nyingi hawaelewi chochote kinachoendelea.

Alisema mama huyo amekimbiwa na mume wake, hivyo amejikuta ndiye anayewalelea watoto wake, hali inayompa ugumu kulingana na kipato chake kuwa duni.

"Nimejisikia vibaya mno kumuona mama huyo anateseka kwa kiasi kikubwa, sina uwezo sana ila nilichokuwa nacho nilijaribu kumsaidia, ili angalau basi kwa siku moja na yeye aweze kupata faraja," alisema Ney wa Mitego.

Hivi karibuni msanii huyo aliingiwa kwenye majozi, baada ya mpenzi wake kumpoteza kichanga chake tumboni, hali ambayo ilimpa simanzi na majonzi.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging