Taasisi ya kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kwa kushirikiana na Bodi ya Ushauri wa Umoja wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Rushwa (AUABC) na Megamark Ltd wameaandaa tamasha kubwa litakalowashirikisha wasanii mbalimbali toka Tanzania, Kenya na Uganda katika kuadhimisha miaka 10 tangu bodi hiyo ya Afrika katika masuala ya Rushwa kuanzishwa.
Msanii Fid Q akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamasha hilo ambapo msanii huyo ni miongoni wa wasanii watakao tumbuiza katika onesho hilo linalotarajia kufanyika Arusha tarehe 7 Decemba katika viwanja vya General Tyre