MUIMBAJI wa nchini Marekani Justin Timberlake amekuwa miongoni mwa wasanii waliovunja rekodi kwa kujinyakulia tuzo tatu katika kinyang'anyiro cha tuzo za Muziki Marekani zilizofanyika Jumapili mwaka huu nchini humo na kuhudhuriwa na wasanii mbalimbali.
Mbali na Justin Timberlake kunyakua tuzo hizo pia wasanii mbalimbali walitunukiwa akiwemo Rihanna, Taylor Swift , Luke Bryan, Marc Anthony na wengine wengi.
Ingawa kwa usiku huo muimbaji Timberlake ameonekana kugang'aa kwa kunyakua tuzo hizo tatu huku akiwa amewabwaga wasanii wenzake ambao walikuwa wapo katika kinyang'anyiro kimoja akiwemo msanii Rihanna ambaye walikuwa wanachuana katika albamu bora ya mwaka.
Katika utoaji wa tuzo hiyo iliambatana na utoaji wa burudani mbalimbali ambapo baaadhi ya wasanii walipata nafasi ya kutoa burudani mahali hapo.
Inadaiwa kuwa muimbaji Lady Gaga ni miongoni mwa watu waliovutia katika kufanya shoo iliyojaa ubunifu ambapo aliimba nyimbo inayojulikana kwa jina la 'Do What You Want' ambayo alishirikiana na R. Kelly .
Show yao hiyo ilianza kwa ubunifu ambapo ilianza kwa mtindo wa igizo, ambapo Gaga aligeuka kuwa 'secretary' na R.Kelly akageuka kuwa rais, tukio ambalo kwa mujibu wa Daily Mail lilirudisha hisia za uhusiano wa miaka 90 kati ya Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton na Monica Lewinsky.