Muongozaji na mtayarishaji wa filamu William John Mtitu amefunguka kwa kusema kuwa awali ametumikishwa sana kwa kufanya kazi kubwa na kutoka jasho bila kuwa na faida ya moja kwa moja kwa kuuza filamu zake kwa wasambazaji ambao utengeneza fedha na kujinufaisha wao badala ya watengene filamu.
Mtitu ambaye anamiliki kampuni ya utengenezaji na kusambaza filamu nchini ya 5 Effects amegundua hilo baada ya kuanza kutengeneza na kusambaza kazi zake bili kupeleka kwa wasambazaji ambao anasema ni wanyonyaji wasio na huruma kwa wasanii, kila wanalalamika kama wanaibiwa lakini anashangaa hawaachi.
“Nawashauri wasanii na watayarishaji wenzangu wenye uwezo kusambaza kazi zao wenyewe badala ya kutegemea wasambaziwe na wasambazaji ambao ununua haki zao na kuwaacha maskini, badala ya kumjengea Mtitu chuki kwa mafanikio ya kupigia moja baada ya kudhulumiwa,”anaongea Mtitu.
Mtitu amewashauri wasanii kuungana na kuanzisha kampuni yao ya usambazaji kwani yeye tayari amefanikiwa na kufanya utafiti baada ya kusambaza filamu zake ambazo ni Omega confusion na Nyati na kuona faida jinsi ilivyo kubwa hivyo kupata imani kuwa wasanii wakisambaza filamu zao wanapata faida kubwa kunufaika na kazi zao.