Google PlusRSS FeedEmail

SITAKI SKENDO ZINIPE UMAARUFU

                                             Asfa Omary
Msanii nyota anayekuja kwa kasi kwenye tasnia ya filamu Hasfa Omary ‘Neema amesema anaogopa mno kupanda skendo katika kazi zake za sanaa kwa kuhofia kuharibikiwa

Alisema tokea anaanza sanaa alijiamini kuwa hatothubutu kufanya skendo ili aweze kujulikana, isipokuwa atahakikisha anafanya vizuri katika kazi zake ili mashabiki wazidi kumkubali kwenye sanaa.

              Asfa Omary
“Nilianza kuingia kwenye sanaa, wazazi wangu walinionya sana kuhusiana na kufanya matukio mabaya kama wanavyofanya wengine ili majina yao yawe makubwa,mimi najiamini kuwa sanaa ukiitumia vizuri bila skendo inaweza kukupa mafanikio makubwa, cha muhimu ni kujituma kwenye kazi zako,” alisema.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging