KIJANA ALIYEPANDA JUKWAANI NA MILEY ATAFUTWA NA POLISI
Kijana aliyekuwa akiishi mitaani, Jesee Helt aliyepanda katika jukwaa la MTV VMAs na Miley Cyrus na kumpokelea tuzo ya video bora ya mwaka anatafutwa na polisi wa Oregon.
Kwa mujibu wa ripoti za mahakama, kijana huyo aliwahi kukamatwa na kufungwa jela siku 30 baada ya kukutwa na hatia ya makosa mbalimbali likiwemo kosa la kuingia kwenye nyumba ya bwana mmoja bila kibali mwaka 2010.
Pamoja na kifungo hicho, kijana huyo ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 18 aliwekwa chini ya kipindi cha matazamio (probation) lakini alivunja masharti baada ya kutoka.
Mahakama ilitoa kibali cha kumkamata tangu mwaka 2011 lakini hawajafanikiwa. Kijana huyo alihamia Los Angeles na kuishi mitaani huku akijaribu kutafuta kazi ya kuwa mwanamitindo.
Miley Cyrus alikutana na kijana huyo katika kituo cha vijana wadogo wanaoishi katika mazingira magumu cha ‘Hollywood homeless Center My Friend’s Place’.
Kijana huyo alipanda jukwaani kupokea tuzo ya Video bora ya mwaka hiyo akiwa na Miley Cyrus (Kumuwakilisha) na alitoa hotuba iliyowagusa wengi kuhusu kuwaangalia vijana wanaoishi katika mazingira magumu.