Google PlusRSS FeedEmail

KARRUECHE AOMBA MSAMAHA



Karrueche Tran amewaomba radhi mashabiki wa Beyonce waliomshambulia kwenye mitandao ya kijamii baada ya kudiss muonekano wa nywele za Blue Ivy kwenye tuzo za MTV VMAs, wakati akifanya kipindi cha 106& Park cha BET.

Karrueche aliponda muonekano wa nywele za Blue Ivy katika kipengele cha kipindi hicho kilichopewa jina la ‘Top 6 Things Blue Ivy thought about the VMA’s’, ambapo alisikika akisema kwa kumkariri Blue Ivy kuwa ‘Kweli niliamka hivi kwa sababu wazazi wangu hawakunichana nywele. Pole Blue! Nakupenda!”

Mashambulizi yaliyoendelea ndani ya siku mbili mfululizo yamemfanya mrembo huyo kuomba radhi kupitia Instagram akikiri kufanya makosa kwa kuwa yeye ni binadamu.

Katika maelezo yake, ameomba radhi kwa kutamka sentensi hiyo ambayo amesema ilitengenezwa kwenye muongozo wa kipindi na BET na ikapitia kwake.

BET wamewajibika pia na kueleza kuwa Karrueche alikuwa anasoma maelezo hayo kwenye teleprompter (screen ya kusomea habari kwenye TV) kama sehemu ya script na kwamba ilifanyiwa mabadiliko dakika kumi kabla ya kwenda hewani na hakupata nafasi ya kuipitia tena.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging