MWANAMITINDO ASHTAKI BAADA YA PICHA ZAKE ZA UTUPU KUTUMIKA
Mwanamitindo Jessie Nizewitz ambaye alikuwa kati ya wasichana waliokuwa kwenye mashindano ya series ya ‘Dating Naked’ amefungua mashitaka dhidi ya makampuni yanayowezesha show hiyo kwa kurusha vipande vinavyomuonesha akiwa mtupu bila kuficha sehemu zake za siri.
Katika shitaka hilo, Jessie anadai fidia ya $10 million kutoka kwa makampuni ya Viacom, Firelight Entertainment, Lighthearted Entertainment kwa kushindwa kuficha kwa kuweka blur kwenye maeneo ya sehemu zake za siri kama walivyokubaliana awali.
“Ingawa niliingia kwenye shindano hilo nikijua kuwa ningeshuti nikiwa mtupu, niliambiwa kuwa sehemu zangu za siri zingefichwa kwa kuwekewa blur kwa ajili ya show ya TV…hata washiriki wengine hawakutegemea kuona hivyo.” Alisema Nizewitz.
Kipande cha show hiyo kinachomuonesha mwanamitindo huyo kilirushwa July 31 mwaka huu.