Msemaji wa Mariah Carey amezungumza kuhusu ndoa ya Mariah na mumewe Nick Cannon ikiwa ni siku chache tangu Nick aweke wazi kuwa walitengana miezi kadhaa iliyopita.
Akiongea na mtandao wa UsMagazine, msemaji huyo wa Mariah ameeleza kuwa hivi sasa mwimbaji huyo amejikita katika tour yake barani Asia na katika kuwaangalia watoto wake mapacha wenye umri wa miaka mitatu, Moroccan na Monroe.
“I don't comment on Mariah's personal life, but Mariah is focusing on her children and her tour.” Ameesema.
Mariah ambaye bado yuko kimya kuhusu suala hilo, anaendelea na tour yake barani Asia na amemaliza kupiga show Tokyo, Japan wikendi iliyopita na anaelekea Manila, Ufilipino ambapo atafanya show October, 28.
Inaaminika kuwa Nick na Mariah walitengana mara baada ya Nick kuweka wazi kupitia kituo cha radio mwezi Machi kuwa aliwahi kuwa na uhusiano na Kim Kardashian na wasichana wengine maarufu.